Magazeti leo Februari 28,2026

Mfumo wa kidijitali wa utoaji wa vyeti vya uasili (Certificate of Origin) kupitia Tanzania Chamber Portal (TCP) unatarajiwa kuanza kutumika rasmi Machi 2, 2026.
Akizungumza mkoani Mbeya wakati wa mafunzo kwa wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi, Makamu wa Rais Kilimo wa Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC), Swallah Swallah, amesema mfumo huo utaongeza uwazi, kasi na ufanisi kwa kupunguza urasimu na muda wa kusubiri, huku ukiimarisha ushindani wa wafanyabiashara katika masoko ya nje.Amesema mfumo huo utapatikana kupitia tovuti ya tcp.tncc.or.tz, kwa lengo la kurahisisha na kuharakisha huduma za biashara za kimataifa nchini na kuhimiza wafanyabiashara kujisajili na kuwasilisha maombi yao mtandaoni ili kunufaika kikamilifu na huduma hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gwakisa Mwaikenda amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha mfumo huo unaunganishwa kikamilifu na mifumo ya forodha ili kurahisisha uthibitishaji na kuharakisha mchakato wa usafirishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here