📌 Wananchi wahamasika kujiunga na huduma ya umeme
📌 Waunga mkono matumizi ya nishati safi ya kupikia
MARA-Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea na ziara ya uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya umeme pamoja na matumizi ya nishati safi ya kupikia mkoani Mara.
Uhamasishaji umehusisha utoaji wa elimu kwa wananachi namna ya kufanya maombi ya kujiunga na huduma ya umeme huku lengo kuu likiwa ni kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme na kuwakumbusha wananchi umuhimu wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Uhamasishaji umehusisha utoaji wa elimu kwa wananachi namna ya kufanya maombi ya kujiunga na huduma ya umeme huku lengo kuu likiwa ni kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme na kuwakumbusha wananchi umuhimu wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.Pia,wakala umefanya kampeni zinazohusisha utoaji wa elimu kuhusu umuhimu na faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo utunzaji wa afya, mazingira pamoja na usawa wa kijinsia.
Aidha, wakala umetoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi bora ya umeme hususani katika shughuli za uzalishaji ikiwemo shughuli za biashara, kilimo na shughuli za nyumbani.
Vile vile,wakala umetoa elimu kuhusu taratibu rahisi za kuomba umeme, Kufundisha umuhimu wa usalama wakati wa matumizi ya umeme, utunzaji wa miundombinu ya umeme na Kuhimiza wananchi kushirikiana na serikali, REA na mkandarasi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

















