Mawaziri wakutana Lushoto kutafuta suluhu ya migogoro ya wananchi mkoani Tanga

TANGA-Mawaziri saba (7) wa kisekta wakiwa na mwenyeji wao ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI,Mhe.Prof.Riziki Shemdoe ambaye ni Mbunge wa Lushoto wamekutana wilayani Lushoto kujadili utatuzi wa changamoto na migogoro inayowakabili wananchi mkoani Tanga ikiwemo ya ardhi, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba aliyoyatoa katika ziara yake ya kikazi inayoendelea mkoani Tanga.
Mwenyekiti wa kikao kazi hicho, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Asiatu Kijaji ameongoza kikao hicho cha viongozi hao na watalaam wa Wizara za Kisekta ambacho kitawasilisha mapendekezo ya utatuzi wa migogoro na changamoto hizo za wananchi kwa Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kabla ya kuhitimisha ziara yake mkoani Tanga, ili kuiwezesha Serikali kuchukua hatua stahiki.
Katika kikao kazi hicho wananchi wenye changamoto mbalimbali wamepata fursa ya kuwasilisha malalamiko yao na kusikilizwa na viongozi hao, ikiwa ni sehemu ya kukiwezesha kikao kazi hicho kuandaa mapendekezo na kutoa ushauri utakaowezesha kupatikana kwa suluhu ya utatuzi wa migogoro na changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili wananchi mkoani humo kwa muda mrefu.

Ili kutatua changamoto na migogoro ya wananchi, Prof. Shemdoe ameshauri wataalamu wa Wizara za Kisekta kuwa na utamaduni wa kuwashirikisha wananchi ili kuepukana na migogoro inayoweza kuepukika kwa ushirikishaji wa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao kazi hicho, Prof. Shemdoe amemshukuru Mhe.Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba kwa kuguswa na changamoto na migogoro inayowakabili wananchi wa Mkoa wa Tanga na hatimaye kuelekeza Mawaziri wa kisekta kukutana Lushoto ili kusikiliza migogoro ya wananchi na kupendekeza namna ya kuitatua.
Mawaziri wengine walioshiriki kikao kazi hicho ni Waziri wa Kilimo na Uvuvi Mhe. Bashiru Ally Kakurwa, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso, Waziri wa Ardhi na Makazi Dkt. Leonard Akwilapo, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde na Naibu Waziri wa Fedha Mhandisi Mshamu Ali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here