Rais Dkt.Mwinyi ashiriki maziko ya mama mzazi wa RC Cassian Nyimbo

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na viongozi, wanafamilia na wananchi mbalimbali katika maziko ya marehemu Theodosia Sylvester Mapunda yaliyofanyika leo Februari 23, 2026.
Marehemu Theodosia Mapunda, ambaye ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mhe. Cassian Gallos Nyimbo, amefariki dunia Februari 21,2026.
Maziko hayo yamefanyika katika Makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi, na yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyama vya siasa pamoja na wananchi.

Akitoa shukrani, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mhe. Cassian Gallos Nyimbo, amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa nia yake njema ya kuwaunganisha Wazanzibari na kuwa wamoja wakati wa faraja na misiba.Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here