Serikali na wadau Iringa wazindua mradi wa kupambana na ugonjwa wa Fistula

IRINGA-Mradi mkubwa wa kupambana na ugonjwa Fistula wenye thamani ya takribani Tsh.Bil.6 umezinduliwa leo Mkoani Iringa kwa lengo la kutoa elimu ya upasuaji wa Fistula kwa wataalam wa Afya pamoja na tiba kwa wagonjwa wa fistula.
Mradi huu mkubwa ujulikanao kama MACORESI utatoa huduma kwa wilaya za Kilolo, Iringa na Mfindi utafanya kazi kwa kushirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali, Chuo cha Elimu ya Afya Muhimbili na shirika la CUAMM Tanzania.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mradi huo leo Februari 18, 2026 mkoani Iringa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt.Silvia Mamkwe aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seifu Shekalaghe amewaambia wajumbe wa mkutano kuwa,  bado wanawake nchini wanateseka kimyakimya kutokana na unyanyapaa, ukosefu wa uelewa na changamoto za upatikanaji wa huduma bora za afya.
Aidha, taarifa ya Katibu Mkuu Shekhalage inabainisha kuwa Tanzania inakadiliwa kuwa kwa mwaka wastani wa wanawake 2,500 hadi 3,000 upata ugonjwa wa fistula wakati wanajifungua na kati yao ni wanawake 1,500 ndio wanaopatiwa matibabu.

Taarifa hiyo imesisitiza uwepo wa takwimu sahihi halisi na mifumo imara ya kukusanya takwimu hizo kwani bila kufanya hivyo ni vigumu kuelewa ukubwa wa tatizo, kupanga na kubaini maeneo yenye hatari zaidi ikiwemo kupima mafanikio kwa ufanisi.

Aidha,Hospitali ya Tosamaganga Iringa ndiyo itakayotumika kituo cha kutoa tiba ya ugonjwa wa fistula kwa Mkoa wa Iringa, hivyo wataalam wa Afya wa hospitali hiyo watapata mafunzo ya namna bora ya kufanya upasuaji wa fistula ikiwemo pia wale wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.

Shirika lisilo la Kiserikali CUAMM linalenga kuimarisha Afya uzazi kwa kuzuia, kupima na kutibu changamoto zinazoweza kujitokeza ili kuzuia fustula ya uzazi ikiwemo kupunguza wakati na kabla ya kujifungua.
Lengo la mradi huu pia nikuja na matokeo ya viwango bora vya afya uzazi, kuongeza helimu ya Afya ya uzazi ikiwemo maandalizi muhimu na viwango vya utoaji huduma kwa mama mjazito.

Ujauzito ni jambo la heshima sana na mtoto ni tunu, mama anapokuwa mjamzito matarajio yake ni kujifungua salama, mwenye afya njema na kubaki salama hivyo kama taifa lazima tuwe na mikakati ya pamoja ili tuweze kutokomeza fistula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here