NA DIRAMAKINI
VILABU vikubwa vya soka Tanzania, Simba Sports Club (Simba SC) na Young Africans Sports Club (Yanga SC) vimeendelea kulitangaza taifa kimataifa baada ya kuingia katika orodha ya vilabu 10 vinavyoongoza barani Afrika kwa idadi ya wafuasi katika mtandao wa Facebook.
Kwa mujibu wa takwimu za karibuni, Simba SC inashika nafasi ya tisa ikiwa na wafuasi milioni 2.8, huku Yanga ikishika nafasi ya kumi kwa wafuasi milioni 2.3.
Mafanikio hayo yanaakisi ukuaji wa soka la Tanzania na kuongezeka kwa mvuto wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kupitia majukwaa ya kidijitali.
Orodha hiyo inaongozwa na klabu ya Al Ahly ya Misri yenye zaidi ya wafuasi milioni 19, ikifuatiwa na Zamalek na Raja Casablanca.
Aidha,uwepo wa Simba na Yanga katika orodha hii unaonesha mchango mkubwa wa mashabiki wao pamoja na ushindani mkubwa uliopo baina ya vilabu hivyo viwili kongwe nchini.
Wachambuzi wa soka wanaeleza kuwa, umaarufu huo ni fursa muhimu kwa vilabu kuongeza mapato ya kibiashara na kuitangaza soka la Tanzania kimataifa.
Nafasi ya tatu inashikiliwa na Raja Casablanca ya Morocco yenye wafuasi milioni 6.4.Kutoka Afrika Kusini, Kaizer Chiefs na Orlando Pirates zinaendelea kudhihirisha nguvu yao ya kihistoria na kibiashara, zikiwa na wafuasi milioni 5.5 na milioni 5 mtawalia.
Wydad Casablanca ya Morocco inashika nafasi ya sita kwa wafuasi milioni 3.9 huku Pyramids FC ikiwa na wafuasi milioni 3.3), Mamelodi Sundowns wafuasi milioni 3.1.
Klabu 10 za Afrika zenye wafuasi wengi Facebook
1️⃣ Al Ahly-19milioni
2️⃣ Zamalek-8.1milioni
3️⃣ Raja-6.4milioni
4️⃣ Kaizer Chiefs-5.5milioni
5️⃣ Orlando Pirates-5milioni
6️⃣ Wydad-3.9 milioni
7️⃣ Pyramids-3.3milioni
8️⃣ Mamelodi Sundowns-3.1milioni
9️⃣ Simba SC-2.8milioni
🔟 Yanga-2.3milioni
