Tanzania yatoa wito wa utulivu, yasisitiza usalama wa raia Mashariki ya Kati

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa matukio yanayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, huku ikisisitiza kuwa inaendelea kufuatilia kwa karibu hali hiyo.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 28,2026 na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Hali ilivyokuwa Bahrain leo baada ya mashambulizi ya Iran. (Picha na Mtandao).

Kupitia taarifa hiyo,Serikali imesema ipo katika mawasiliano ya mara kwa mara na Balozi zake zilizoko katika eneo husika ili kutathmini hali inavyoendelea na kulinda maslahi ya Taifa pamoja na usalama wa raia wake.

Pia,wizara hiyo imewataka Watanzania wanaoishi au kusafiri katika maeneo yaliyoathirika kuwa makini, kuweka usalama wao mbele, na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na mamlaka za nchi husika pamoja na Ofisi za Kibalozi za Tanzania.

Aidha, Tanzania imesisitiza msimamo wake wa kuunga mkono juhudi za jumuiya ya kimataifa katika kuhimiza uvumilivu, kupunguza mvutano, na kutafuta suluhu ya amani katika migogoro kwa kuzingatia misingi ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here