Ushaidi wa tunda la mti wa kati kuliwa Ngorongoro huu hapa

ARUSHA-Mwaka 1976, Mtafiti wa masuala ya Akiolojia Dr. Mary Leakey aligundua nyayo za zamadamu eneo la Laetoli zilizohifadhika katika mwamba wa jivu la volcano iliyolipuka kwenye milima ya Ngorongoro zaidi ya miaka milion 3.6 iliyopita.
Wataalamu wanaamini kuwa nyayo hizo ziliachwa na jamii ya watu wa kale waitwao Australopithecus Afarensis.

Nyayo za Zamadamu Laetoli Ngorongoro ni ushahidi usiopingika kuwa zamadamu (Hominin) wa umri wa miaka milioni 3.66 iliyopita walitembea wima kwa miguu miwili eneo la Laetoli Tanzania.

Kutembea wima kwa miguu miwili kunatutofautisha wanadamu na wanyama kama Sokwe na Nyani waliotokana na babu/bibi mmoja miaka takribani millioni 7 iliyopita.

Uwepo wa Nyayo na masalia ya binadamu, ndege na wanyama, urithi wa utamaduni, mambo kale, mimea, maji, matunda na kila kitu kinachomfanya binadamu kuishi ni kiashiria kuwa pengine bustani ya Eden ni Ngorongoro ni mahali ambapo tunda la mti wa katikati lililiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here