Waziri wa Fedha ashiriki Futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameshiriki Futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB katika ukumbi wa SuperDome, jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo imewakutanisha viongozi wa serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo na baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuendeleza umoja wa kitaifa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Katika tukio hilo, Mhe. Balozi Omar pia alikabidhi zawadi kwa watu wenye mahitaji maalum walioko katika baadhi ya vituo vya kulelea watoto kama ishara ya upendo, mshikamano na utu wema unaohimizwa katika kipindi cha Ramadhani.

Mheshimiwa Balozi Omar aliwapongeza NMB kwa mchango wao katika jamii na kuendelea kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua maisha ya wananchi na akatoa wito kwa taasisi, kampuni, mashirika na wadau wengine kuiga utamaduni wa NMB wa kutambua mchango wa wadau wao na kuonesha upendo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here