Waziri Mavunde akutana na wadau wa kimataifa INDABA kuvutia uwekezaji

CAPE TOWN-Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde anayeongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Kongamano la Mining Indaba akiongozana na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Msafiri Mbibo na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Mhe. James Bwana wamefanya vikao vya pembeni Februari 9, 2026 na viongozi, wawekezaji na kampuni kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kuboresha mahusiano, kuvutia uwekezaji na kukuza sekta ya madini nchini Tanzania.
1. 𝙈𝙆𝙐𝙏𝘼𝙉𝙊 𝙉𝘼 𝙒𝘼𝙕𝙄𝙍𝙄 𝙒𝘼 𝙈𝘼𝙎𝙐𝘼𝙇𝘼 𝙔𝘼 𝘽𝙄𝘼𝙎𝙃𝘼𝙍𝘼 𝙉𝘼 𝙐𝘾𝙃𝙐𝙈𝙄 𝙒𝘼 𝙁𝙄𝙉𝙇𝘼𝙉𝘿 𝙈𝙃E. 𝙎𝘼𝙆𝘼𝙍𝙄 𝙋𝙐𝙄𝙎𝙏O

Mkutano huu umelenga kuimarisha ushirikiano baina ya Taasisi ya Jiolojia ya Finland (GTK) na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kupitia MoU ili:-

■ Kuwajengea uwezo watalaamu katika kuchambua, kutafsiri na kuhakiki ubora wa taarifa za Jiosayansi nchini Tanzania.

■ Kujenga uwezo wa watalaamu wa GST katika kuendesha maabara hususan upimaji wa sampuli kwa viwango vya kimataifa.

■ Kushirikiana kwenye Utafiti wa jiosayansi hususan High Resolution Geophysical Surveys.

2. KIKAO NA TAASISI MBALIMBALI KUTOKA SERIKALI YA MAREKANI

Ujumbe wa Taasisi kutoka Nchini Marekani uliongozwa na Naibu Mkurugenzi na Mkuu wa Shughuli za Uendeshaji za Shirika la Maendeleo ya Biashara la Watu wa Marekani (USTDA), Bw. Thomas Hardy.
Kikao hicho kimejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Marekani na Tanzania ikiwemo:-

■ Utafiti na uongezaji thamani wa madini muhimu na madini mkakati nchini Tanzania.

■ Umuhimu wa tafiti za kina za jiosayansi zinazohusisha kurusha ndege.

■ Maendeleo ya mradi wa utafiti wa madini ya kinywe kwa kushirikiana na GST katika leseni zinazomilikiwa na STAMICO.

■ Umuhimu wa uongezaji thamani madini ndani ya nchi kwa mujibu wa Sheria ya Madini, Sura 123.
Mhe. Waziri ameeleza umuhimu wa kufanya tafiti za kina na kusisitiza kuwa ni vyema Serikali ya Marekani ikaweka mkazo katika eneo hili ili kuwezesha uanzishwaji wa miradi mingi kwenye sekta ya madini nchini.

Aidha, Mhe. Mavunde amebainisha kuwa, utaratibu wa kufanya tafiti za kina kwa kushirikiana na GST ukawa endelevu ili kupata taarifa zaidi za kina za kuwezesha kuanzisha miradi mikubwa ya uchimbaji madini.

3. MKUTANO NA TAASISI YA RIO TINTO YENYE UZOEFU WA ZAIDI YA MIAKA 150 KATIKA SEKTA

Uwepo wa miundombinu ya Reli ya Kisasa (SGR) Shirika la Pamoja la Serikali ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Sera ya Madini, mazingira wezeshi ya kibiashara Sekta ya Madini Tanzania yametajwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyoivuta Kampuni ya Kimataifa ya Rio Tinto yenye uzoefu wa miaka 150 kwenye shughuli za madini kuonesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini nchini.
Kampuni hiyo inafanya shughuli zake katika nchi takribani 35 duniani na imejikita katika utafiti na mnyororo wa thamani wa madini ya Shaba, Bauxite Aluminium na Graphite. Mhe.Mavunde amesisitiza kuwa;

■ Rio Tinto imeshauriwa kuwezesha kufanyika utafiti kwa haraka na ifanye mazungumzo na STAMICO ambao wanamiliki leseni za utafiti kwenye madini wenye uhitaji nayo ili wafanye kwa pamoja na kuwezesha kuanza shughuli za uchimbaji kwa wakati.
■Kwa mujibu wa Sheria, STAMICO wanaruhusiwa kuingia ubia na wawekezaji ndani na nje ya nchi, hivyo Rio Tinto wana nafasi kubwa na wanakaribishwa nchini Tanzania ili kuwekeza kwenye utafiti na baadaye kuanzisha mgodi wa kimkakati ambao utahusisha ujenzi wa kiwanda cha kuongeza thamani ya madini hayo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here