Waziri Mavunde,wataalam wajadili mikakati kuongeza mapato ya Serikali na manufaa zaidi ya sekta

DODOMA-Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Februari 16, 2026 ameongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Madini, Taasisi na wataalam kujadili mikakati ya namna bora ya kuongeza mapato ya Serikali yatokanayo na rasilimali madini kwa lengo la kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa, uchumi, ustawi wa jamii na kuwezesha miradi mingine ya maendeleo.Aidha, kikao hicho kimejadili mikakati madhubuti ya kuendeleza Sekta ya madini ili kuongeza tija zaidi na manufaa ya rasilimali madini kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Dira ya Madini 2030 inayolenga kufanya tafiti za kina za madini angalau kufikia asilimia 50 kutoka 16 ya sasa na Ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) za Mwaka 2025-30 katika Sekta ya Madini.
Mbali na wataalam hao, kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here