DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewaahidi wawekezaji kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya uwekezaji nchini kwa manufaa ya pande zote mbili kutokana na manufaa ya sekta hiyo kwa uchumi wa nchi na wawekezaji.
Mheshimiwa Balozi Omar amesema hayo mjini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni mpya ya Uchimbaji Dhahabu Nyanzaga (Nyanzaga Mining Company Ltd), unaojengwa katika eneo la Nyanzaga Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ambao hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 523.
Mheshimiwa Balozi Omar amesema hayo mjini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni mpya ya Uchimbaji Dhahabu Nyanzaga (Nyanzaga Mining Company Ltd), unaojengwa katika eneo la Nyanzaga Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ambao hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 523.Alisema kuwa,mradi huo ni mkubwa kujengwa Tanzania toka miaka zaidi ya 18 iliyopita ambapo mgodi wa Buzwagi ulijengwa.
Na fursa zitaendelea hivyo kwa ukubwa wake. Lakini pia kuchangia uchumi wa nchi Kupitia kodi mbalimbali.
“Ni mara yangu ya kwanza kukutana na uongozi wa mgodi wa dhahabu wa Nyanzagi na tumejadili kuhusu changamoto ya msamaha wa kodi na nimewaahidi kuwa hadi mwisho wa mwezi Februari, 2026, tutahakikisha changamoto hiyo inafanyiwa kazi kwankishirikiana na wadau wote wanaohusika,” alisema Mhe. Balozi Omar.
Akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa Mgodi huo, Meneja Mtendaji wa Ndani wa mradi wa Nyanzaga, Bw. Isaac Lupokela, aliishukuru Serikali Kupitia Waziri wa Fedha, kwa namna inavyoshughulikia masuala ya kufanikisha biashara na uwekezaji nchini.
Alisema kuwa, Mgodi wa Dhahabu wa Nyanzaga, unatarajiwa kuanza uzalishaji ifikapo robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027.
Alisema kuwa Mmradi huo mpaka sasa wakati shughuli za ujenzi zinaendelea umetoa fursa za ajira za moja kwa moja na kupitia makandarasi takribani 2,000 ambao zaidi ya 80% ni Watanzania.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Sera za Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya, na kwa upande wa mwekezaji, walikuwepo Bi Lee-Anne de Bruin - Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni Mama ya Australia (Perseus Mining Limited) na Mwneja Mkuu wa Ujenzi wa Mgodi wa Nyanzaga Bw. Matt Cavedon

