Wizara ya Afya yaandaa ujumbe wa utoaji elimu kuhusu Vidonge vya Virutubishi vya Nyongeza (MMS) kwa Mama wajawazito nchini

MOROGORO-Wataalamu wa Afya wanakutana kwa siku tatu Manispaa ya Morogoro kuandaa ujumbe wa utoaji elimu kwa umma kuhusu Virutubisho vya Nyongeza (MMS) kwa mjawazito nchini.
Lengo la kikao hiki ni kuwashirikisha wadau muhimu ili kuandaa kwa pamoja ujumbe wa namna bora ya kuhakikisha jamii ya watanzania wanapata uelewa wa matumizi ya Vidonge vya Virutubishi vya Nyongeza ambavyo vikitumika ipasavyo uchangia kupunguza madhara yatokanayo na changamoto za uzazi ikiwemo upungufu wa damu kwa mama mjamzito.
Mtaalam wa semina hiyo elekezi ni Dkt. Phineas Sospiter Mratibu wa Uzazi Salama Idara ya Afya ya Uzazi Salama kutoka Wizara ya Afya ambaye anaongoza jopo la wataalam kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja OWM- TAMISEMI wanaokaa kwa siku tatu kuandaa mwongozo wa mpango wa elimu kwa umma kuhusu vidonge hivyo.
Dkt. Sospiter wakati akiwasilisha mada yake kwa ujumbe huo alibainisha kuwa takwimu za WHO zinaonesha 40% ya mama wajawazito nchini wanakuwa na changamoto ya upungufu wa damu (Anemia) kipindi cha ujauzito, ambapo suala hili linapelekea umuhimu wa matumizi ya vidonge hivyo kwa wajawazito.
Matumizi ya mapema ya vidonge vya Virutubishi vya Nyongeza (MMS) upunguza uwezekano wa mjamzito kujifungua mtoto mwenye ulemavu wa kichwa kikubwa, mgongo wazi pamoja na mdomo.

Vidonge vya Kuongeza Virutubishi (MMS) vina virutubishi vya lishe vinavyotolewa kwa mjazito kwa lengo la kuzuia au kutibu upungufu wa damu na kuimarisha afya ya mjamzito kabla na baada ya kujifungua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here