BASATA yamfungia msanii Halima Kibaokata miaka mitatu

DAR-Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia msanii Halima Haji, maarufu kama Halima Kibaokata, kujihusisha na shughuli za sanaa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia leo Machi 21, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa ya BASATA, hatua hiyo imetolewa kufuatia msanii huyo kusambaza kipande cha video ya muziki kinachodaiwa kukiuka maadili ya Mtanzania.

BASATA imesema baada ya tathmini ya kina imethibitisha kuwa Halima ametenda makosa ya kimaadili kwa makusudi.

Aidha, imebainika kuwa Halima amekuwa akijishughulisha na kazi za sanaa bila kusajiliwa rasmi na BASATA, kinyume na taratibu.

Kutokana na makosa hayo, msanii huyo ametakiwa kuondoa mara moja video husika kwenye mitandao yote ya kijamii na kulipa faini ya shilingi milioni tatu ndani ya siku 14 kuanzia leo.

BASATA imeeleza kuwa video husika ina maudhui yanayokiuka maadili, ikiwemo lugha ya matusi na maneno yanayodhalilisha, hali inayodaiwa kuathiri heshima ya jamii, wimbo na hadhira kwa ujumla.

Baraza limekumbusha wasanii wote kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya maadili katika uzalishaji na usambazaji wa kazi za sanaa, huku likisisitiza kuwa sanaa ni ajira, biashara na chombo cha maendeleo ya jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here