Wizara ya Fedha yatoa maelekezo mapya kwa taasisi kuhusu Bajeti ya muda wa kati mwaka 2026/2027-2028/2029

DODOMA-Timu ya watalam kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, Wizara ya Fedha, imezitaka Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuzingatia maelekezo yaliyopo kwenye mwongozo wa maandalizi ya mipango na bajeti wa Serikali wa muda wa kati 2026/2027-2028/2029 na kuhakikisha kuwa msisitizo unawekwa katika ukamilishwaji wa miradi inayoendelea.
Waliyasema hayo wakati wa kikao kazi kilichowahusisha wataalam wa Wizara, kwa ajili ya kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.
Katika kikao hicho, wataalam walipata nafasi ya kujadili kwa kina namna bajeti zinavyoweza kuyafikia malengo yaliyowekwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kuimarisha uchumi wa Taifa na kuchochea maendeleo endelevu na kukusitizwa kuzingatia kipaumbele katika shughuli za msingi katika kila sekta ili shughuli hizo ziweze kutekelezwa kwa wakati.

Kikao hicho kiliongozwa na Kamishna Msaidizi, Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Fundi Makama na kuhudhuriwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Andambike Mololo, Wakurugenzi wa Sera na Mipango pamoja na wataalamu kutoka wizara na sekta husika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here