DIRAMAKINI yawatakia Waislamu na Watanzania wote Sikukuu njema ya Eid El-Fitri

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa Kampuni ya Diramakini Business Limited (DIRAMAKINI) umetuma salamu za heri na pongezi kwa Waislamu wote nchini na duniani kwa ujumla katika kusherehekea Sikukuu ya Eid el-Fitri, ikiashiria kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Katika salamu hizo, kampuni hiyo ambayo ni wamiliki wa tovuti ya habari ya www.diramakini.co.tz imeeleza kuwa, kipindi cha Ramadhani kimekuwa cha kipekee kwa Waislamu, kikiambatana na ibada, kujitafakari, na kuimarisha mshikamano wa kijamii.

Uongozi umepongeza waumini wa dini ya Kiislamu kwa uvumilivu, nidhamu na moyo wa kujitoa waliouonesha katika kipindi chote cha mfungo.

Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri Mkuu wa DIRAMAKINI, Godfrey Ismaely Nnko amesema kuwa, Eid el-Fitri ni fursa muhimu ya kuendeleza maadili mema yaliyopatikana wakati wa Ramadhani na kuyafanya kuwa sehemu ya maisha ya kila siku.

“Ninapenda kuchukua fursa hii kuwatakia Waislamu wote Eid el-Fitri njema iliyojaa furaha, amani na baraka tele. Tunatambua mchango mkubwa wa jamii ya Kiislamu katika kulinda maadili, kusaidia wahitaji, na kuimarisha mshikamano katika jamii yetu,” amesema Godfrey Ismaely Nnko.

Ameongeza kuwa,DIRAMAKINI inaamini katika umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania wa dini na makundi mbalimbali, akisisitiza kuwa, maadhimisho ya sikukuu hii yawe chachu ya kuendeleza amani na utulivu nchini.

“Tunawaomba Watanzania wote kuendelea kudumisha amani, kuheshimiana, na kushirikiana katika kujenga taifa lenye mshikamano na maendeleo endelevu. Sikukuu hii iwe ni wakati wa kuimarisha mahusiano ya kifamilia na kijamii,” aliongeza.

Kwa upande mwingine, kampuni hiyo imewahimiza wananchi kusherehekea sikukuu hiyo kwa tahadhari, kuzingatia usalama wao na wa wengine hususan kipindi hiki ambacho maeneo mengi ya nchi yanashuhudia mvua kubwa, pamoja na kuendelea kusaidiana hasa kwa makundi yenye uhitaji.

Aidha,uongozi wa DIRAMAKINI umehitimisha kwa kuwatakia Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla Sikukuu njema ya Eid el-Fitri yenye heri, afya njema na mafanikio katika maisha yao ya kila siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here