Elimu ya kidijitali ni nguzo ya maendeleo Zanzibar-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya FMSS Bilişim Teknolojia ya Uturuki, ndugu Cihan Aktaş pamoja na ujumbe wake, waliofika Ikulu Zanzibar leo Machi 26,2026.Rais Dkt.Mwinyi ameihakikishia kampuni hiyo ushirikiano katika kufanikisha dhamira yake ya kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuleta mageuzi ya mfumo wa kidijitali katika sekta ya elimu Zanzibar, na kueleza kuwa elimu ni sekta ya kipaumbele kwa maendeleo ya Zanzibar.
Aidha, ameiagiza Wizara ya Elimu kuendelea na mazungumzo na kampuni hiyo ili kubaini maeneo muhimu ya ushirikiano katika sekta ya elimu, akisisitiza kuwa mbali na kuimarisha elimu, hatua hiyo itaongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya Zanzibar na Uturuki.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya FMSS Bilişim Teknolojia ya Uturuki, Ndugu Cihan Aktaş, amesema kampuni hiyo imeamua kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuleta mageuzi katika sekta ya elimu Zanzibar kwa kutumia mfumo wa elimu ya kidijitali.
Ameeleza kuwa,kampuni hiyo ina uzoefu wa muda mrefu katika mafunzo kwa walimu, teknolojia, ufundishaji na amepongeza hatua iliyofikiwa katika maendeleo ya kielimu Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here