ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Uhakiki wa Rasimu ya Pili ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II), utakaofanyika kesho tarehe 27 Machi 2026, kuanzia saa 2:30 asubuhi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
