MANYARA-Mahakama ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara imetoa hukumu ya kifungo cha moaka 30 jela kwa mshtakiwa Kepa Heha maarufu kama Bachani baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kuzini na Maharimu ambaye ni mtoto wake wa kumzaa (jina tunalihifadhi) mkazi wa Mtaa wa Komoto wilayani humo kinyume cha sheria.
Awali imeelezwa mahakamani hapo na waendesha Mashtaka Rwezaula na Miss Leah toka Ofisi ya Taifa ya Mashistaka kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Februari 16, 2026 huko katika mtaa wa Komoto Kata ya Bagara Tarafa ya Babati Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara.
Akisoma hukumu hiyo Machi 26, 2026 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoa Manyara, Mhe. Massao ameeleza kuwa, Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo ambao umemuunganisha mtuhumiwa kutenda kosa hilo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
