Kamati ya Bunge yakagua maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Mzumbe Tanga

TANGA-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Michezo na Utamaduni, tarehe 13 Machi 2026 imefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Tanga ya Chuo Kikuu Mzumbe inayotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (Higher Education for Economic TransformationHEET).
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko (Mb) akiongoza Wajumbe wa Kamati hiyo kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Tanga, unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

Ziara hiyo imelenga kufuatilia utekelezaji wa mradi huo pamoja na kukusanya taarifa zitakazosaidia katika maandalizi ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027, hususan katika kuimarisha uwekezaji katika miundombinu ya elimu ya juu nchini.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozana na viongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe, timu ya mkandarasi pamoja na mshauri elekezi wa mradi, wakikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Tanga.
Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu yaangazia Maendeleo ya Mradi wa Kampasi ya Mzumbe Tanga.

Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Sekiboko, akiambatana na Makamu Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa kamati hiyo. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Sekiboko alipongeza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo na kusisitiza umuhimu wa kuhakikisha kazi zote zilizopangwa zinakamilika kwa wakati kwa kuzingatia masharti ya mkataba na matarajio ya Serikali.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Adolf Faustine Mkenda alisema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya elimu ya juu kupitia miradi ya kimkakati ikiwemo HEET, kwa lengo la kuongeza fursa za elimu, utafiti na ubunifu zitakazochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

Awali akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi huo kwa kamati hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha alisema, utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali umefikia takribani asilimia 82. Alieleza kuwa, miundombinu inayojengwa ni pamoja na jengo la taaluma, kituo cha afya, mabweni ya wanafunzi, mgahawa, nyumba za wafanyakazi pamoja na mifumo ya maji safi na maji taka.
Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu yaangazia Maendeleo ya Mradi wa Kampasi ya Mzumbe Tanga.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo yaridhishwa na Maendeleo ya ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Tanga.

Katika ziara hiyo, wajumbe wa kamati pamoja na viongozi wa Wilaya ya Mkinga na Mkoa wa Tanga walipata fursa ya kutoa maoni na ushauri kuhusu maendeleo ya mradi huo, wakieleza kuwa kukamilika kwa kampasi hiyo kutachochea ongezeko la fursa za elimu pamoja na kuvutia shughuli za uwekezaji zinazowesha kuchangia moja kwa moja katika maendeleo pamoja na kuimarisha shughuli za kiuchumi na kuongeza fursa za ajira katika ukanda wa Tanga na maeneo jirani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here