DAR-Kamishna Jenerali Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo leo Machi 28,2026 amesaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), marehemu Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Lukuvi amefariki dunia Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.
DCEA, itamkumbuka Mhe. Lukuvi kwa ushauri wake katika uratibu wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Tags
Aretas Lyimo
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kamishna Jenerali Aretas Lyimo
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)
