Taifa laomboleza:Rais Dkt.Samia aeleza mchango mkubwa wa William Lukuvi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Machi 28,2026 ameongoza viongozi wa kitaifa, familia, na wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge na Wenye Ulemavu), Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi, katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwafariji wafiwa mara baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam tarehe 28 Machi, 2026.
Rais Dkt.Samia amesema, Taifa limepoteza kiongozi mwenye uzoefu mkubwa na aliyetoa mchango wa muda mrefu katika utumishi wa umma, akimtaja Marehemu Lukuvi kuwa miongoni mwa viongozi waliolitumikia Taifa kwa uzalendo, bidii na uadilifu.

“Tumeondokewa na kiongozi wetu, ndugu yetu na mtumishi mwenzetu aliyejitolea maisha yake kwa Taifa. Msiba huu si wa familia pekee bali ni wetu sote Watanzania, kwa sababu wengi waliguswa na mchango wake katika utumishi wa umma,” amesema Rais Dkt.Samia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwaongoza Watanzania kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi, tarehe 28 Machi, 2026.

Aidha, Rais Dkt. Samia amesema marehemu Lukuvi atakumbukwa kwa busara zake, uzoefu mkubwa wa uongozi na mchango wake katika kuimarisha uratibu wa shughuli za Serikali, ikiwemo kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kushughulikia changamoto za wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Ameongeza kuwa,Taifa limepoteza William Lukuvi katika kipindi kilichohitaji uzoefu, hekima na ushauri wake, hasusan katika wakati uliopo wa changamoto za kiuchumi na kisiasa duniani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam tarehe 28 Machi, 2026.

“Katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali, tulimhitaji ndugu Lukuvi zaidi kuliko wakati wowote kutokana na uzoefu wake mkubwa katika uongozi wa Taifa,” amesema Rais Dkt. Samia na kuongeza kuwa utumishi wake unabaki kuwa mfano wa uongozi wa kujitolea, na kuwahimiza viongozi na watumishi wa umma kuendeleza misingi ya uwajibikaji, uzalendo na kujitoa kwa manufaa ya Taifa.

Rais Dkt.Samia pia amesema,marehemu Lukuvi alikuwa kiongozi aliyegusa maisha ya wananchi wengi kupitia mtindo wake wa uongozi wa kusikiliza, kushauri na kuchukua maamuzi kwa maslahi ya Taifa.

Familia ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi, ikiwa kwenye Misa takatifu ya kumuombea Marehemu katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Machi, 2026.
Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wakiwa kwenye Misa takatifu ya kumuombea aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Machi, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waombolezaji kabla ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam tarehe 28 Machi, 2026.
Familia ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi, ikiwa kwenye Misa takatifu ya kumuombea Marehemu katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Machi, 2026.
Familia ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi, ikiwa kwenye Misa takatifu ya kumuombea Marehemu katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Machi, 2026.
Familia ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi, ikiwa kwenye Misa takatifu ya kumuombea Marehemu katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Machi, 2026.

Ameeleza kuwa, uzoefu wake wa muda mrefu katika nyadhifa mbalimbali za Serikali, Bunge na Chama cha Mapinduzi ulimfanya kuwa miongoni mwa viongozi waliokuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha utendaji wa Serikali.

Aidha, Rais Dkt. Samia amesisitiza kuwa, utumishi wa marehemu Lukuvi ni kielelezo cha uongozi wa kujitolea, akibainisha kuwa viongozi na watumishi wa umma wanapaswa kuendeleza misingi ya uwajibikaji, uzalendo na kujitoa kwa manufaa ya Taifa kama alivyofanya marehemu katika kipindi chote cha utumishi wake.

Awali, akisoma wasifu wa Marehemu, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi, amesema Marehemu Lukuvi, aliyeshika nyadhifa mbalimbali za uongozi enzi za uhai wake, alitambulika kwa uchapakazi na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake, hususan katika kuratibu shughuli za Serikali, na kuongeza kuwa atakumbukwa kwa mchango wake katika kuimarisha uhusiano kati ya Serikali na Bunge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya kuwaongoza Watanzania kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na wenye Ulemavu), Hayati William Vangimembe Lukuvi, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam tarehe 28 Machi, 2026.

Ibada ya kuaga pia imeshuhudiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi, pamoja na viongozi wengine wakuu na wastaafu wa Serikali, sekta binafsi, vyama vya siasa, viongozi wa dini, pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here