Katibu Mkuu wa UVCCM,Halid Mwinyi asaini kitabu cha maombolezo msiba wa Waziri Lukuvi

DODOMA-Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC) leo Machi 26, 2026 amesaini kitabu cha maombolezo kufuatia msiba wa William Vangimembe Lukuvi aliyekuwa Mbunge wa Isimani na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu) nyumbani kwake Area D jijini Dodoma.
Enzi za uhai wake Mhe. Lukuvi alihudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi UVCCM akiwa Katibu wa UVCCM wilaya za Masasi, Mtwara, Arusha na Dodoma.
Pia amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu na Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa. Alikuwa Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni UVCCM, Katibu wa UVCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam na mwisho alikuwa Naibu Katibu Mkuu-UVCCM.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here