Ratiba ya msiba wa marehemu William Vangimembe Lukuvi

Akisoma ratiba ya mazishi, Ofisa Mwandamizi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anayeshughulikia Habari, Mawasiliano na Elimu kwa Umma, Patson Sobha amesema kabla ya maziko, marehemu Lukuvi ataagwa katika Viwanja vya Bunge kesho Ijumaa, Machi 27, 2026 kuanzia asubuhi na kisha kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.

Akiwa Dar es Salaam, marehemu Lukuvi ataagwa katika Viwanja vya Karimjee siku ya Jumamosi, Machi 28, 2026 na kusafirishwa kwenda Iringa ambako pia ataagwa katika eneo la Gangilonga siku ya Jumapili, Machi 28, 2026 na kisha kusafirishwa kwenda Idodi kwa ajili ya maziko.

Siku ya Jumanne, Machi 31, 2026 hatimaye mwili wa marehemu William Lukuvi utapumzishwa katika makaburi ya nyumbani kwake, Idodi mkoani Iringa.

Ratiba ya msiba wa marehemu William Vangimembe Lukuvi (MB) na aliyekuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Machi 27 hadi 31,2026 (Dodoma, Dar es Salaam na Iringa);


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here