Mbibo atembelea maduka ya bidhaa za mapambo ya usonara Arusha

ARUSHA-Leo Machi 31, 2026, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo ametembelea maduka (vituo vya kutangazia bidhaa za Vito na Usonara zinazozalishwa na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) vilivyopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC jijini Arusha ili kujionea bidhaa za mapambo ya vito na usonara zinazouzwa katika vituo hivyo viwili.
Vilevile, Naibu Katibu Mkuu Mbibo, amepata nafasi ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo pacha la ghorofa Nane la TGC l kutumia wasaa huo kuzungumza na watumishi wa TGC huku akiwahimiza kutafiti na kuja na bunifu zitakazoongeza tija kwenye bidhaa zinazozalishwa sasa, kufuatia kuwepo ushindani mkubwa wa kibiashara uliopo sokoni unaotokana na kukua kwa kasi ya teknolojia za vifaa na ujuzi unaotumiwa na nchi za nyingine zilizobobea katika shughuli za uongezaji thamani madini ikiwemo India, Thailand, China na nyingine.
Vilevile, amewahimiza watumishi wa TGC kuiendeleza hali yao ya sasa ya uadilifu na moyo wa kujituma bila kujali changamoto ndogo zinazowakabili kwenye mazingira yao ya kazi.

Mwisho amehitimisha kwa kuwakumbusha kuweka vizuri taarifa za kazi wanazozifanya ili wapate wepesi wa kuzirejea wakati wa utekelezaji na pia kuwezesha utendaji wenye ufanisi.
Kituo cha TGC, kipo chini ya Wizara ya Madini kilichopo jijini Arusha kinatoa mafunzo ya uongezaji thamani madini ya vito na miamba katika fani mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here