Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki ibada ya mazishi ya Waziri Lukuvi mkoani Iringa

IRINGA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Hamza Johari leo Machi 31, 2026 ameshiriki ibada ya mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Vangimembe Lukuvi yaliyofanyika katika Kijiji cha Idodi, mkoani Iringa.
Ibada hiyo ya mazishi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, ndugu, jamaa na wananchi waliokusanyika kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Lukuvi, aliyekuwa kiongozi mashuhuri na aliyetoa mchango mkubwa katika utumishi wa umma.

Aidha,ibada ya mazishi iliongozwa na Naibu Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Padre Paul Msombe ambaye alisisitiza kuwa ni vema watu wakaishi huku wakijiandaa kwa maisha ya baadaye mbinguni.

Lukuvi alifariki dunia Machi 25, 2026, alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Kifo cha Lukuvi kimeelezwa kuwa ni pengo kubwa kwa Taifa, hususan kutokana na mchango wake katika uongozi, utungaji wa sera na uwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Isimani.

Maziko ya marehemu yamefanyika nyumbani kwake, katika Kijiji cha Idodi, ambapo amezikwa katika eneo la makaburi ya familia, kufuatia ibada ya kumuaga iliyoambatana na salamu za rambirambi kutoka kwa viongozi na wananchi walioguswa na msiba huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here