SINGIDA-Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Mhe. Jesca Kishoa, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwa kuanzisha Kliniki Tembezi ya kutoa elimu kuhusu mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Pongezi hizo amezitoa tarehe 16 Machi 2026 wakati wa uzinduzi wa Kliniki Tembezi ya “Mkalama Asilimia 10 Kliniki (MAK)” uliofanyika katika Kata ya Nkalakala, Wilaya ya Mkalama.
Pongezi hizo amezitoa tarehe 16 Machi 2026 wakati wa uzinduzi wa Kliniki Tembezi ya “Mkalama Asilimia 10 Kliniki (MAK)” uliofanyika katika Kata ya Nkalakala, Wilaya ya Mkalama.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Kishoa amesema ubunifu huo utasaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na kuwapatia elimu sahihi kuhusu namna ya kuomba, kusimamia na kutumia mikopo hiyo kwa ajili ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi.Akiwasilisha kuhusu hali ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Asia J. Mesos, amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri tayari imetoa jumla ya shilingi milioni 290 kuanzia mwezi Julai 2025 hadi Januari 2026 kwa vikundi 35 vya wajasiriamali.
Kliniki hiyo tembezi inatarajiwa kupita katika kata zote 17 za Wilaya ya Mkalama ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi kuhusu mikopo ya asilimia 10 na namna bora ya kunufaika na fursa hiyo.
