NA DIRAMAKINI
YOUNG Africans Sports Club (Yanga SC) imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara (NBC Premier League) msimu wa 2025/2026 baada ya kukusanya pointi 32 katika michezo 12 iliyocheza.
Kwa mujibu wa jedwali la ligi hiyo, Young Africans imeonesha ubora mkubwa kwa kushinda michezo 10 na kutoka sare mbili bila kupoteza hata mmoja, huku ikipeleka wavuni mabao 30 na kuruhusu mabao mawili pekee.Nafasi ya pili inashikiliwa na JKT Tanzania yenye pointi 28 baada ya kucheza michezo 17, ikishinda saba, kutoka sare saba na kupoteza mitatu.
Katika nafasi ya tatu ipo Azam FC yenye pointi 24 baada ya michezo 12, sawa na pointi za Simba SC iliyopo nafasi ya nne lakini ikiwa imecheza michezo 11 pekee.
Timu nyingine zinazofuata katika nafasi za juu ni Pamba Jiji FC yenye pointi 24 katika michezo 15, huku Namungo FC, Dodoma Jiji FC na Mtibwa Sugar zikifuatia kwa pointi 21 kila moja.
Kwa upande wa katikati ya msimamo, Singida Black Stars ipo nafasi ya tisa ikiwa na pointi 19, ikifuatiwa na Mashujaa FC yenye pointi 17 pamoja na TRA United SC yenye pointi 16.
Timu za Coastal Union na Fountain Gate FC zinashika nafasi za 12 na 13 kwa pointi 15 kila moja.
Katika ukanda wa hatari wa kushuka daraja, Mbeya City FC na Tanzania Prisons zipo na pointi 13 kila moja, huku KMC FC ikishika mkia wa msimamo ikiwa na pointi nane baada ya michezo 16.