MUWSA yatangaza zawadi ya shilingi milioni mbili kwa atakayefichua wizi wa Mita za Maji

KILIMANJARO-Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) imetangaza kutoa zawadi ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kwa mwananchi yeyote atakayetoa taarifa sahihi zitakazosaidia kubaini na kuwakamata wahusika wa vitendo vya wizi wa mita za maji na uharibifu wa miundombinu ya maji katika eneo lake la huduma.
Uamuzi huo umetokana na kuongezeka kwa matukio ya hujuma yanayohusisha wizi wa mita za maji, viungio vyake, mifuniko ya chemba za maji pamoja na gate valve, hali inayohatarisha upatikanaji wa huduma bora ya maji kwa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka hiyo, jumla ya mita 266 zimeibwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi, 2026 katika kata za Makuyuni, Njiapanda, Majengo na Mwika Kaskazini, pamoja na maeneo ya jirani.

Matukio hayo yamesababisha hasara inayokadiriwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 37.24 kwa Serikali.

MUWSA imewahakikishia wananchi kuwa taarifa zote zitakazotolewa zitashughulikiwa kwa umakini mkubwa na kwa usiri wa hali ya juu ili kulinda usalama wa watoa taarifa, huku ikisisitiza kuwa ushirikiano wa jamii ni muhimu katika kukomesha vitendo hivyo vya uharibifu wa miundombinu ya umma.

Kwa ajili ya kuwasilisha taarifa, mamlaka imetenga namba maalum ya simu: 0791 992 525, ambayo itatumika kupokea taarifa za vitendo vya hujuma na wizi wa miundombinu ya maji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here