Naibu Waziri Maghembe afanya mazungumzo na Naibu Waziri Moraka jijini Pretoria

PRETORIA-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe amefanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Thandi Moraka pembezoni mwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Pretoria Machi 13, 2026.
Mazungumzo hayo ambayo yalihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha. Mhe. Laurent Luswetula na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. James Bwana yalijadili namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushiririkiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Afrika Kusini, nchi ambazo zina uhusiano wa kihistoria wa muda mrefu.
Moja ya hatua ambazo viongozi hao wamekubaliana ni kuongeza kasi ya kukamilisha rasimu za Hati za makubaliano katika maeneo mbalimbali ili ziweze kusainiwa na kutekelezwa kwa manufaa ya pande zote mbili.

Mhe. Maghembe alipongeza nchi ya Afrika Kusini kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa nchi 20 tajiri zaidi duniani (G20) mwaka 2025 na maandalizi mazuri ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri la SADC uliofanyika kwa siku mbili Machi 12 na 13, 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here