Profesa Shemdoe kuzifanyia kazi changamoto za wafanyabiashara Soko la Mabibo

DAR-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Mhe.Prof. Riziki Shemdoe amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutatua mgogoro uliopo katika soko hilo.
Akizungumza na wafanyabiashara hao Machi 4, 2026 katika ofisi ndogo za OWM-TAMISEMI Magogoni jijini Dar es Slaam, Prof. Shemdoe amesema,yuko tayari kutatua changamoto za wafanyabiashara walizoziwasilisha kwake ambazo ni pamoja na kurejeshwa katika soko hilo baada ya kuzuiliwa na uongozi wa soko, kurudishiwa vizimba vya biashara na ombi la kutaka usimamizi wa soko hilo kujeshwa kwa wafanyabiashara wa Mabibo.
Prof. Shemdoe ameahidi kushughulikia maombi ya wafanyabiashara hao ndani ya wiki mbili na kuwaahidi kukutana tena baada ya kupata ufumbuzi wa suala hilo.

Aidha, Prof.Shemdoe ameteua kamati Maalum ya kushughulikia suala hilo chini ya uenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu anayeshugulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila.
Hatua ya Prof. Shemdoe inafuatia maelekezo aliyoyatoa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mwigulu Nchemba baada ya wafanyabiashara hao kuwasilisha changamoto hizo kwake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here