Rais Dkt.Mwinyi asisitiza uwajibikaji na ushirikiano wa wadau kufanikisha MKUMBI-II

DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI-II), ili kuharakisha kufikiwa kwa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Akizungumza katika Mkutano wa Uhakiki wa Rasimu ya MKUMBI-II uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) leo Machi 27,2026 jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa, kufikia uchumi wa kipato cha juu ifikapo mwaka 2050 kunahitaji ukuaji wa uchumi wa wastani wa asilimia 10 kwa mwaka, sambamba na uwekezaji mkubwa katika sekta za uzalishaji.
Ameeleza kuwa, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa kufanya mapitio ya sheria, kupunguza tozo na kodi, pamoja na kuimarisha miundombinu na mifumo ya TEHAMA, hatua ambazo zimeanza kuzaa matokeo chanya katika kuvutia uwekezaji na kuongeza ajira.
Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi amebainisha kuwa mafanikio ya MKUMBI-II yatategemea uwajibikaji wa pamoja, ushirikiano endelevu na matumizi ya teknolojia za kisasa, huku akiwahimiza wadau kutoa maoni yatakayoboresha rasimu hiyo kabla ya utekelezaji wake rasmi.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Sekta binafsi na Wadau wa Maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here