Makamu wa Rais Dkt.Nchimbi ateta na Mfalme wa Eswatini mjini Malabo

MALABO-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akifanya mazungumzo na Mfalme wa Eswatini, Mswati III kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki, unaofanyika Malabo nchini Guinea ya Ikweta leo Machi 27,2026.
Mazungumzo hayo yamelenga namna ya kukuza na kuimarisha ushirikiano, kuchochea maendeleo na mageuzi ya Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) ili kuweza kukabiliana na changamoto na mahitaji ya sasa.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. James Milya, Balozi wa Tanzania Guinea ya Ikweta mwenye makazi yake Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo Mhe. Said Juma Mshana pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Umoja wa Ulaya Mhe. Jestas Nyamanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here