ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na viongozi wa dini na masheikh waliofika Ikulu leo, tarehe 21 Machi 2026, mara baada ya Sala ya Eid al-Fitr.
Wakati huohuo, Rais Dkt. Mwinyi ametoa Mkono wa Eid kwa mamia ya watoto na wananchi, wakiwemo wajane na wenye mahitaji maalum waliofika Ikulu. Aidha, Alhaj Dkt. Mwinyi amewatakia heri na baraka katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el-Fitr.
Rais Dkt. Mwinyi ameendelea na utaratibu wake wa kudumu wa kutoa Mkono wa Eid kwa watu wa makundi maalum pamoja na watoto wakati wa Sikukuu hiyo.















