NA DIRAMAKINI
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema inafuatilia kwa karibu hali ya usalama inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati.


Kutokana na mazingira ya kiusalama yanayoendelea, Serikali imetoa ushauri kwa raia wa Tanzania wanaoishi au wanaopanga kusafiri kwenda katika eneo hilo, ikiwemo Bahrain, Israel, Kuwait, Qatar,Falme za Kiarabu (UAE) na Oman.Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 3,2026 na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
"Serikali inapenda kuwajulisha wananchi kuwa, kwa nyakati kama hizi, usaidizi wa
kibalozi ana kwa ana unaweza kuwa na mipaka kulingana na eneo alipo mhusika na hali halisi ya kiusalama. Hivyo, raia wote wanahimizwa kuchukua tahadhari stahiki na kufuata maelekezo ya mamlaka husika."
Watanzania waliopo katika eneo la Mashariki ya Kati wanashauriwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
■Kuepuka kufanya safari za kwenda au kutoka Mashariki ya Kati katika kipindi hiki.
■Kubaki katika makazi mnayoishi inapowezekana.
■Kufuata maagizo yanayotolewa na mamlaka za maeneo husika na kuwa waangalifu wakati wote.
■Kuepuka maeneo yenye shughuli za usalama/kijeshi katika maeneo mnayoishi.
■Kutumia njia rasmi za mawasiliano na taarifa.
■Kuhifadhi pasipoti na vitambulisho vya Tanzania sehemu salama na inayopatikana haraka endapo kutatokea dharura.
"Serikali inawasihi Watanzania walioko Mashariki ya Kati kujisitiri kwa uangalifu na
kuendelea kufuatilia mawasiliano rasmi ya Ubalozi na ya dharura."
Aidha, Watanzania wanaombwa kujisitiri kwa usajili kupitia kiunganishi kifuatacho kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu:
https://www.foreign.go.tz/forms/diaspora_middle_east_registration
Kwa dharura au maswali zaidi, wasiliana na Ubalozi wa Tanzania ulio karibu kama ifuatavyo;
1:Ubalozi wa Tanzania-Kuwait City, KUWAIT
WhatsApp: +965 517 51892
Simu: (+965) 22 575 367 / (+965) 22 575 368
Barua pepe: kuwait@nje.go.tz
2:Ubalozi wa Tanzania-Doha, QATAR
Simu: (+974) 40360860 / (+974) 40360863
Barua pepe: doha@nje.go.tz
3:Ubalozi wa Tanzania-Abu Dhabi, UAE
Simu: +971 2 6313088
WhatsApp: +971 5 01601829 / +971 543116380
Barua pepe: abudhabi@nje.go.tz
4:Ubalozi wa Tanzania-Riyadh, Saudi Arabia
WhatsApp: +966 58 220 0369
Simu: +966 (11) 454 2833
Barua pepe: info@tanzaniaembassy.org.sa | riyadh@nje.go.tz
5:Ubalozi wa Tanzania-Tel Aviv, ISRAEL
Simu: (+972) 3-776-1100
WhatsApp: +972 52 829 5946
Barua pepe: telaviv@nje.go.tz
Nakala: tztelaviv@gmail.com
6:Ubalozi wa Tanzania-Ankara, Uturuki
Simu: +90 312 490 10 61
WhatsApp: +255 623 881 570
Barua pepe: ankara@nje.go.tz
"Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na
Misheni za Kidiplomasia itaendelea kutoa taarifa na usaidizi wa kibalozi kadri hali
itakavyoruhusu katika maeneo husika."