ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi amekutana na uongozi wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) uliofika ofisini kwake Ikulu, Migombani tarehe 30 Machi 2026.
Ujumbe huo ulioongozwa na Rais wa chama hicho, Dkt. Mary Mwanyika Sando.
Aidha, Mama Mariam Mwinyi amewashukuru MEWATA kwa kuonesha dhamira yao ya kushirikiana na ZMBF katika masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya afya, elimu ya lishe , na tafiti mbalimbali kuhusu zao la Mwani.
Vilevile, ameeleza kuwa ZMBF iko tayari kushirikiana na MEWATA katika nyanja mbalimbali hizo.
Naye, Rais wa MEWATA,Dkt.Mary Mwanyika amempongeza Mama Mariam Mwinyi kwa mafanikio makubwa aliyoyapata kupitia Taasisi yake ya ZMBF kwa kuwafikia Wananchi katika Kambi mbalimbali za Matibabu na uchunguzi wa afya zilizofanyika chini ya uratibu wa ZMBF, kuwasaidia kuwainua Wanawake kiuchumi hususan Wakulima wa Mwani, kuwasaidia Wasichana Taulo za kike aina ya Tumaini, elimu ya lishe na kuhamasisha kufanya mazoezi katika kupambana na Magonjwa yasiyoambukiza. 

Halikadhalika, MEWATA wamemualika Mama Mariam Mwinyi kushiriki mkutano wa Madaktari Wanawake Afrika utaokaofanyika Zanzibar tarehe 05 Mei mwaka 2027 .
Vilevile, amefahamisha kuwa MEWATA iko tayari kushirikiana na ZMBF katika programu mbalimbali.
Tags
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Habari
Mama Mariam Mwinyi
MEWATA Tanzania
Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)


