Tanzania yaendelea kung’ara kimataifa katika sayansi ya hali ya hewa

NA DIRAMAKINI

TANZANIA imeendelea kujipambanua kimataifa katika sekta ya hali ya hewa kupitia ushiriki wa wataalamu wake katika mashirika ya kimataifa huku wakitoa matokeo chanya katika nafasi zao.
Akitoa ujumbe rasmi wa maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani Machi 23, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt.Ladislaus Benedict Chang’a amesema, kaulimbiu ya mwaka huu, “Pima hali ya hewa leo, ili kesho iwe salama,” inalenga kuhimiza matumizi sahihi ya data za hali ya hewa katika kufanya maamuzi yenye tija kwa maendeleo endelevu.

Dkt. Chang’a ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC) amesema, wataalamu wa Tanzania wanahudumu katika kamati mbalimbali za Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Jopo la IPCC.

Vilevile, TMA pia imeendelea kushikilia cheti cha ubora cha ISO 9001:2015 katika utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga, na hivyo kuendelea kuthibitisha ubora wa huduma mahususi za hali ya hewa kwa ajili usafiri wa anga.

"Kwa upande wa ushiriki katika mchango wetu wa kimataifa, TMA imeendelea kuiwakilisha Tanzania ipasavyo katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa ambapo wataalamu 15 wa Tanzania wanahudumu katika vikosi kazi vya kamati mbalimbali za Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) pamoja na Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (IPCC). "

Kwa mfano Dkt. Ladislaus Chang’a, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, alichaguliwa mwezi Julai 2023 kuwa Makamu Mwenyekiti wa IPCC kwa kipindi cha miaka saba.

Aidha, Dkt.Pascal Waniha, Mkurugenzi wa Miundombinu wa Huduma za Ufundi wa TMA, anahudumu kama Makamu Rais wa Kamisheni ya WMO ya uangazi, miundombinu ya data na taarifa za hali ya hewa (WMO Commission on Observation, Infrastructure, and Information Systems-INFCOM) tangu mwaka 2024.

Pia,Dkt.Hamza Kabelwa, Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, anahudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ya WMO inayoshughulikia mfumo jumlishi wa WMO wa uchakataji wa taarifa za hali ya hewa na utabiri (WMO Standing Committee on WMO Integrated Processing and Prediction System (SC-WIPPS)) tangu mwaka 2024.

"Ushiriki wa wataalamu hawa katika ngazi za vyombo hivi vya kimataifa ni kudhihirisha mchango mkubwa wa Tanzania katika kuanua na kutelekeza kanuni za miongozo ya utoaji wa huduma za hali ya hewa duniani."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here