TMA yaadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani, yaahidi kuimarisha mifumo ya tahadhari

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeungana na jumuiya ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani leo Machi 23, 2026, huku ikisisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya uangazi wa hali ya hewa kwa ajili ya kulinda maisha na mali.
Akitoa ujumbe rasmi wa maadhimisho hayo leo Machi 23, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt.Ladislaus Benedict Chang’a amesema, kaulimbiu ya mwaka huu, “Pima hali ya hewa leo, ili kesho iwe salama,” inalenga kuhimiza matumizi sahihi ya data za hali ya hewa katika kufanya maamuzi yenye tija kwa maendeleo endelevu.

Dkt. Chang’a ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC) amesema,Tanzania inaendelea kuimarisha huduma za hali ya hewa kupitia uwekezaji wa kimkakati unaohusisha ununuzi wa vifaa vya kisasa, ujenzi wa miundombinu pamoja na matumizi ya teknolojia ya hali ya juu.

“Serikali imewekeza katika rada tano za hali ya hewa na inaendelea kuboresha mifumo ya utabiri ili kuongeza usahihi wa taarifa na tahadhari za mapema,” amesema Dkt. Chang’a.

Ameongeza kuwa,mifumo hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya watu na kusaidia sekta mbalimbali za uchumi, zikiwemo kilimo, usafiri na uvuvi.

TMA ikiwa ni Mamlaka ya Kitaifa yenye jukumu la kutoa huduma maalum kwa ajili ya hewa kwa umma, taasisi mbalimbali na watumiaji binafsi wa huduma maalum kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Sambamba na kusimamia na kuratibu shughuli za hali ya hewa katika mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoa tahadhari na ushauri kuhusu matukio ya hali mbaya ya hewa kwa lengo la kulinda maisha ya watu na mali zao, inaunga na jumuiya ya hali ya hewa duniani kote kuadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani kwa mwaka 2026.

Maadhimisho ya mwaka huu ni kumbukizi ya miaka 76 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) tarehe 23 Machi 1950.

Tanzania ni mwanachama wa nchi wanachama 193 wa WMO, ambapo kupitia TMA inaendelea kuthibitisha dhamira yake thabiti ya kuimarisha huduma za hali ya hewa ambazo ni msingi muhimu wa usalama, ustawi wa jamii na maendeleo endelevu ya taifa.

Kaulimbiu ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani mwaka huu ni: “Pima hali ya hewa leo, ili kesho iwe salama” (Observing Today, Protecting Tomorrow).

Kaulimbiu hii inalenga kusisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya uangazi wa hali ya hewa na matumizi sahihi ya data ya hali ya hewa zinazokusanywa ili kuwezesha maamuzi yenye tija katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Taarifa hizi zimeendelea kusaidia kuongeza uelewa shajati, usalama na ustahimilivu wa jamii yetu kwa sasa na kwa vizazi vijavyo.

"Kaulimbiu hii pia inatukumbusha sisi wataalamu wa hali ya hewa, wanasayansi, watafiti na wadau mbalimbali kuwa, uangazi na ufuatiliaji wa mifumo ya hali ya hewa ni msingi wa kazi zote tunazoifanya.

"Kuanzia vituo vya uangazi wa ardhini na anga za juu, RADA na mitandao ya uangazi wa maji, mifumo hii hutuwezesha kuelewa mienendo ya mifumo ya hali ya hewa, kutambua hatari zinazoweza kujitokeza, na kutoa taarifa sahihi za hali ya hewa pamoja na tahadhari za mapema kwa wakati muafaka."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here