DAR-Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba amewataka Wanawake wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutumia Jukwaa la Wanawake na Kodi lililozinduliwa hivi karibuni kuelimisha wajasiriamali wanawake kuhusu umuhimu wa kujisajili, kuwasilisha taarifa sahihi na kulipa kodi kwa wakati.
Dkt. Mwamba ametoa wito huo wakati akizungumza na wanawake wa TRA, katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw.Yusuph Juma Mwenda, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania,Bw. Mcha Hassan Mcha, Kaimu Mkurugenzi Usimamizi Rasilimali watu na Utalawa Bw. Nahoda Pandu Nahoda.







