Wadau watathmini uandaaji wa Sera ya Usimamizi wa Mali za Umma nchini

DODOMA-Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, imefanya kikao cha tathmini ya kina kwa wadau kuhusu uandaaji wa Sera ya Usimamizi wa Mali za Umma nchini.
HKatika kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kambarage, Wizara ya Fedha, jijini Dodoma, washiriki walijadiliana na kuwasilisha maoni yao kuhusu sera itakayoandaliwa.

Kikao hicho kiliwakutanisha Wakurugenzi Wasaidizi, Wasimamizi wa Mali za Serikali wa Mikoa, Maafisa Ununuzi, Wahasibu, Wakaguzi, Wazee wa Mkoa wa Dodoma, wajasiriamali, baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na mwakilishi wa vijana kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.
Kikao hicho kilifunguliwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Chotto Sendo, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua na kilifungwa na Mkurugenzi msaidizi wa Usimamizi wa Mifumo na Mali, Wizara ya Fedha, Bw. Ismael Nehemia Ogaga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here