Wanawake wa Kikundi cha Wasikivu wawezeshwa na TASAF ili kuinua uchumi wao


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza mara baada ya kuwasili kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Kiwanda cha kutengeneza Siagi kinachomilikiwa na kikundi cha Wasikivu TASAF kilichopo Mtaa wa Igombe, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (wa kwanza kulia) akiwasili na sehemu ya Wajumbe wa Kamati hiyo Mtaa wa Igombe, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza kwa lengo la kukagua utekelezaji wa mradi wa Kiwanda cha kutengeneza Siagi kinachomilikiwa na kikundi cha Wasikivu TASAF.
Mwonekano wa sabuni za vipande na sabuni za maji ambazo zinatengenezwa na Kikundi cha Wasikivu TASAF ambapo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imefanya ziara ya kikazi katika eneo hilo iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Kiwanda cha kutengeneza Siagi kilichopo Mtaa wa Igombe, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (wa pili kutoka kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza kutoka kushoto) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kikundi cha Wasikivu TASAF, Bi. Laurencia Lugendo (wa kwanza kulia) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Kikundi hicho kwa Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Kiwanda cha kutengeneza Siagi kilichopo Mtaa wa Igombe, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akitoa maelezo ya awali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Kiwanda cha kutengeneza Siagi kinachomilikiwa na kikundi cha Wasikivu TASAF kilichopo Mtaa wa Igombe, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifurahia jambo pamoja na Wanakikundi cha Wasikivu TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi wa Kiwanda cha kutengeneza Siagi kilichopo Mtaa wa Igombe, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, mkoani Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here