Wanawake wa TMA waadhimisha Siku ya Wanawake Duniani 2026 kwa kufanya shughuli za kijamii

DODOMA-Wanawake wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa kufanya shughuli tofauti za kijamii zinazolenga kuimarisha mshikamano na kusaidia jamii.
Maadhimisho hayo yalifanyika kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo: “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana; Msingi Jumuishi kufikia Dira ya Maendeleo 2050.”
Katika Mkoa wa Dodoma, watumishi wanawake wa TMA walipata fursa ya kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha Safina kilichopo Ntyuka, ambapo walikutana na watoto wanaolelewa katika kituo hicho na kuwapa faraja pamoja na kuwasaidia kwa mahitaji mbalimbali.

Ziara hiyo ililenga kuonesha upendo, mshikamano na kuwapa matumaini watoto wasiokuwa na wazazi au wale wanaoishi katika mazingira magumu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here