Waziri wa Fedha aialika Italia kuongeza uwekezaji na kushiriki miradi mikubwa Tanzania

DAR-Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na mataifa mbalimbali na kukaribisha uwekezaji pamoja na kukuza biashara kwa manufaa ya pande zote.
Mhe. Balozi Omar amesema hayo, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Giusseppe Coppola, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.

Alieleza kuwa tangu mwaka 2011, nchi hizi mbili zimefanikiwa kutekeleza miradi minne mikubwa ya ushirikiano yenye thamani ya zaidi ya euro milioni 509, katika sekta za kuimarisha mifumo ya takwimu, programu za elimu ya ufundi, pamoja na mchango kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (European Development Fund).
Miongoni mwa mafanikio muhimu ni kuboreshwa kwa taasisi kama Chuo cha Ufundi Arusha, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT). Aidha, Italia imechangia katika kupanua huduma za usajili wa vizazi, hususan usajili wa watoto chini ya miaka mitano katika mamia ya vituo vya afya na kata nchini.

Aidha, katika kuimarisha zaidi ushirikiano huo, Mhe. Balozi Omar ameiomba Italia kuongeza msaada kupitia bajeti, misaada ya kiufundi na uwekezaji pamoja na kuihimiza Italia kuendelea kushiriki katika miradi mikubwa ya kimkakati kama ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge (SGR).
Kwa upande wake Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Giusseppe Coppola, alisema kuwa nchi yake inathamini ushirikiano imara uliopo kati ya nchi hizo mbili na kuahidi kuuendeleza.

Alisema kuwa juhudi kubwa zinahitajika katika kukuza biashara na uwekezaji na kwamba baadhi ya kampuni zilizowekeza nchini katika sekta za mvinyo na madini zimetambuiiwa kuwa miongini mwa walipakodi wakubwa.

Mhe. Balozi Coppola alisema kuwa Italia iko tayari kuendelea kuchangia marndeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo, hifadhi ya mazingira, uongezaji thamani wa mazao ya kilimo (kahawa), Tehama na ukuzaji biashara.
Kikao hicho kilihuhudhuriwa pia na Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melkzedeck Mbise na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na wawakilishi wa Ubalozi wa Italia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here