Waziri wa Fedha aipongeza Azania Bank kwa kuchochea ukuaji wa uchumi nchini

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amesema kuwa, Serikali inafuatilia kwa karibu mienendo ya biashara ya sekta ya fedha hususan benki na kuridhishwa na udhibiti wa mikopo isiyolipika (mikopo chechefu) pamoja na uwezeshaji wa mikopo katika sekta binafsi hatua inayochangia kuchachua uchumi wa nchi.
Mhe. Balozi Omar amesema hayo alipokutana na Menejimenti ya Benki ya Azania PLC, ikiongozwa na Mkurugenzi wake Mtendaji, Dkt. Esther Mang’enya iliyofika kujitambulisha katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Mtaa wa Madaraka jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, katika siku za hivi karibuni, Benki mbalimbali zimekuwa zikitangaza faida pamoja na kudhibiti mikopo chechefu jambo ambalo ni zuri kwa upande wa wawekezaji kwa kuwa wanapata faida ya uwekezaji na kuondoa vihatarishi vinavyoweza kuathiri ufanisi wa Taasisi hizo huku wananchi.
Mhe. Balozi Omar ameipongeza Azania Bank Plc, moja ya benki kubwa inayomilikiwa na Watanzania kupitia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na wadau wengine, kwa kuendelea kuimarisha nafasi yake katika sekta ya fedha nchini kwa kutoa mchango mkubwa katika kukuza ujumuishaji wa huduma za kifedha, kusaidia sekta binafsi, na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Akitoa taarifa ya Benki hiyo Mkurugenzi Mtendaji wake, Dkt. Esther Mang’enya alisema kuwa katika mwaka wa fedha ulioishia Desemba 2025, Benki ya Azania iliorodhesha mali zenye thamani ya takribani sh. trilioni 3.68, amana za wateja (deposits) zenye thamani ya sh. trilioni 2.50 na kutoa mikopo yenye thamani ya sh. trilioni 2.59 na kupata faida baada ya kodi kiasi cha sh. bilioni 57.56.
Amesema kuwa,benki hiyo pia ilidumisha kiwango cha mtaji (capital adequacy ratio) cha asilimia 17.19, kikubwa kuliko kiwango cha chini kinachohitajika na mdhibiti (Benki Kuu ya Tanzaniai, huku mikopo isiyolipika (mikopo chechefu) ikiwa ni asilimia 1.76 pekee.

Kwa ukubwa wa mali, Benki ya Azania inasalia kuwa miongoni mwa mabenki ya kati (mid-tier banks) yanayoongoza nchini na kushika nafasi ya nne miongoni mwa benki zinazofanya vizuri nchini, ikiimarisha nafasi yake ya kuwa taasisi muhimu katika upanuzi wa utoaji mikopo na ufadhili wa biashara.
Benki ya Azania imejijengea umaarufu kama benki thabiti ya wazawa inayochangia kwa kiasi kikubwa kwenye ukuaji wa sekta ya fedha, kusaidia biashara na kuwezesha wananchi kupata huduma bora za kifedha.
Kupitia ushirikiano na mifuko ya hifadhi ya jamii na uwekezaji endelevu katika teknolojia na huduma jumuishi, benki hiyo inaendelea kuwa nguzo muhimu ya uchumi na maendeleo ya Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here