Waziri wa Fedha aongoza majadiliano ya Serikali na Fitch Ratings kuhusu Uchumi wa Tanzania

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameongoza kikao cha mapitio ya kwanza ya mwaka 2026 kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Kimataifa inayojihusisha na kutathimi uwezo wa nchi kuyafikia masoko ya Kimataifa ya mitaji na dhamana ya Fitch Ratings Ltd, kuhusu uwezo wa nchi kukopa na kukopesheka katika masoko ya fedha ya kimataifa.
Mapitio na majadiliano hayo yameanza leo tarehe 16 Machi, 2026, jijini Dar es Salaam na yataendelea hadi tarehe 18 Machi, 2026, kwa kufanya majadiliano ya kina na Wizara, taasisi za Serikali na sekta binafsi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha mapitio, Mhe. Balozi Omar alieleza kuwa,uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa makisio ya asilimia 6, hali inayodhihirisha uimara wa Sera za kiuchumi pamoja na jitihada za Serikali katika kuimarisha sekta mbalimbali za uchumi.
Kwa upande wa Fitch, majadiliano haya yanalenga kuwapa fursa ya kupata taarifa za kina kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania, Sera za fedha na mikakati ya Serikali katika usimamizi wa deni la taifa.

Aidha, majadiliano hayo yanalenga kuimarisha uwazi na upatikanaji wa taarifa kwa wawekezaji wa kimataifa, pamoja na kuongeza uaminifu wa masoko ya fedha kuhusu uwezo wa nchi kukopa na kukopesheka.

Baada ya mapitio hayo, Kampuni hiyo itatoa matokeo ambayo ni muhimu katika kuimarisha uwazi na upatikanaji wa taarifa kwa wawekezaji wa kimataifa, pamoja na kuongeza uaminifu wa masoko ya fedha kuhusu uwezo wa nchi kukopa na kukopesheka.
Kikao hicho kiliwashirikisha pia, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Wizara ya Fedha anayesimamia Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bw. Japhet Justine, Kaimu Kamishna wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. Remidius Ruhunduka, Viongozi wengine na Maafisa wa Serikali, Wizara ya Fedha, ambapo Ujumbe wa Fitch Rating ulishiriki kikao hicho kwa njia ya mtandao wa zoom kutokea nchini Marekani, ukiongozwa na Chief Analyst, Bw. Jose Mantero.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here