DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amekutana kwa mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Standard and Poor’s (S&P) inayojihusisha na kufanya tathmini ya uwezo wa nchi kukopesheka na kuyafikia Masoko ya Mitaji ya Kimataifa.

Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake wa Kanda ya Afrika-nchini Afrika Kusini, Bi. Samira Mensah, akiambatana na Mkurugenzi Mshirika wa masuala ya biashara Idara ya Afrika wa taasisi hiyo, Bw. Raiston Muller, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, iliyoko Mtaa wa Madaraka jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, mazungumzo yalijikita namna ya kufanya kazi na Tanzania.

