TAKUKURU yatangaza nafasi 500 za ajira kwa Watanzania

NA DIRAMAKINI

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imetangaza nafasi za ajira kwa nafasi za Afisa Mchunguzi (250) na Mchunguzi Msaidizi (250) ikiwa ni mahususi kwa Watanzania wenye sifa za kitaaluma na uzoefu ili kuhudumu katika ofisi za TAKUKURU wilaya nchini.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TAKUKURU, nafasi hizo zinapatikana kwa waombaji wenye shahada za kwanza, stashahada, na vyeti kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha,waombaji wanatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 29, na waombaji wa nafasi ya Mchunguzi Msaidizi wanapaswa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 25.

Waombaji wa nafasi za Mchunguzi wanatakiwa kuwa na shahada ya kwanza katika mojawapo ya fani zifuatazo: uhasibu, uchumi, sheria, usimamizi wa biashara, sayansi ya kompyuta (TEHAMA), na uhandisi. Aidha, waombaji wanatakiwa kuwa na ujuzi wa kutumia kompyuta na vifaa vya ofisi.

Kwa upande wa nafasi za Msaidizi, waombaji wanahitaji kuwa na cheti au stashahada katika fani mbalimbali kama vile uhasibu, utawala, sheria, na sayansi ya jamii. Pia, waombaji wanapaswa kuwa na ujuzi wa matumizi ya kompyuta na vifaa vya ofisi kama printer na photocopier.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here