Serikali yatoa rai kwa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini

NA SAIDINA MSANGI,
WF

SERIKALI imetoa rai kwa wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuimarisha mahusiano ya kikazi kati ya Serikali na wadau hao, pamoja na kuongeza uwazi, uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika warsha ya siku moja iliyokutanisha washiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mwanza, Pwani, Mtwara, Kagera na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Rai hiyo ilitolewa na Kaimu Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. John Kuchaka, wakati akifungua warsha ya siku moja iliyokutanisha washiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mwanza, Pwani, Mtwara, Kagera na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Alisema warsha hiyo itawezesha washiriki kuelewa kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali hapa nchini ili kuimarisha ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kijamii.
Kaimu Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. John Kuchaka, akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja iliyokutanisha washiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mwanza, Pwani, Mtwara, Kagera na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.

‘‘Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa maendeleo ya wananchi yanapatikana kwa njia jumuishi na endelevu, hivyo mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali ni muhimu sana, hasa katika kufikisha huduma kwa jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta mbalimbali,’’ alisema Bw. Kuchaka.
Afisa Usimamizi wa Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Omar Mkima, akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha ya siku moja iliyokutanisha washiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mwanza, Pwani, Mtwara, Kagera na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Bw. Kuchaka alisema kuwa ni muhimu kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mifumo, taratibu na miongozo inayosimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ili kuwezesha ushirikiano huo uwe na tija na kufikia malengo.

‘‘Wadau wote ni muhimu kuelewa miongozo muhimu ikiwemo Mwongozo wa uzingatiaji fedha na ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali, Mwongozo wa Bajeti ya Serikali pamoja na Miongozo ya uratibu na ushirikiano wa maendeleo, hivyo kupitia warsha hii tunatarajia sote kujenga uelewa wa pamoja,’’ alisema Bw. Kuchaka.
Afisa Usimamizi wa Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Doroth Lihweuli, akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo wa uzingatiaji fedha na ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali, katika warsha ya siku moja iliyokutanisha washiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mwanza, Pwani, Mtwara, Kagera na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.
Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum (Ofisi ya Msajili wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali), Abraham Mushashu, akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali, katika mafunzo yaliyoratibiwa na Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, kwa lengo la kujenga uelewa na kubadilishana uzoefu kuhusu ushirikiano wa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Alisisitiza washiriki wa warsha hiyo kutumia fursa ya mafunzo kubaini maeneo yanayohitaji maboresho ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Baadhi ya washiriki wakichangia hoja kuhusu mada zilizowasilishwa katika mafunzo yaliyoratibiwa na Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, kwa lengo la kujenga uelewa na kubadilishana uzoefu kuhusu ushirikiano wa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa warsha hiyo, Katibu Mkuu Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Bi. Fransisca Mboya, Kupitia warsha hiyo wamejifunza namna bora ya kuwasilisha shughuli na mchango wa mashirika yao ili yatambulike zaidi kitaifa kwa kazi wanayofanya, hususan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na utoaji wa huduma kwa jamii.
Katibu Mkuu Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Bi. Fransisca Mboya, akizungumza baada ya kuhitimishwa kwa warsha ya ya siku moja iliyokutanisha washiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mwanza, Pwani, Mtwara, Kagera na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.

‘‘Tumefurahia majadiliano na mada zilizowasilishwa na mwisho tumetoa mapendekezo yetu ya namna bora ya kuboresha mahusiano kati ya mashirika yasiyo ya serikali kwa pamoja na Serikali’’, alisema Bi. Mboya.
Kaimu Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. John Kuchaka (katikati),akiwa katika picha ya pamoja washhiriki baada ya katika warsha ya siku moja iliyokutanisha washiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mwanza, Pwani, Mtwara, Kagera na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Aidha, walitoa rai kuwa mafunzo kama hayo yawe endelevu ili kuendelea kuwajengea uwezo wadau wote hasa katika masuala ya usimamizi wa fedha, hatua itakayohakikisha kuna kuwa na ushirikiano imara na endelevu katika kuleta mabadiliko chanya ya kijamii na kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here