Mashindano ya Qur'an yanaimarisha maadili na kukuza vipaji vya vijana-Rais Dkt.Mwinyi

DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa mashindano ya kuhifadhi Qur’an yamekuwa chachu ya kuibua vipaji vya vijana pamoja na kukuza maadili mema katika jamii.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Aprili 5,2026 katika dhifa ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Jumuiya ya Tuzo za Kimataifa za Kuhifadhi Qur’an Tukufu, iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa mashindano ya kuhifadhi Qur’an siyo tu mashindano ya Kitabu Kitukufu, bali pia ni kielelezo cha kuitambulisha Tanzania yenye amani duniani kote.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Taasisi ya Tuzo za Kuhifadhi Qur’an Tanzania chini ya uongozi wa Sheikh Othman Ali Kaporo kwa kuendeleza mashindano hayo kwa mafanikio, pamoja na kuandaa dhifa hiyo ya chakula cha usiku kwa washiriki.

Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ni mgeni maalum, Sheikh wa Msikiti wa Al-Haram wa Makkah, Sheikh Badr bin Muhammad Al-Turki, pamoja na Balozi wa Saudi Arabia nchini. Mhe. Yahya Bin Ahmed Okeish.

Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’an yamefanyika Aprili 5,2026 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo mshiriki kutoka Libya, Ibrahim Hilal Zeydaan, amekuwa mshindi wa kwanza kwa kupata pointi 99.12. Mshindi wa pili ni Saydina Al Ghalla kutoka Mauritania aliyepata pointi 99.06, na mshindi wa tatu ni Ahmed Karim Shehmadduf kutoka Urusi aliyepata pointi 98.75.
Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi ametunukiwa tuzo mbili maalum za kutambua juhudi na mchango wake katika kuendeleza masuala ya dini ya Kiislamu nchini, zilizotolewa na Ubalozi wa Saudi Arabia na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here