Msanii Harmonize akiri kudaiwa kodi ya nyumba,ahamia Goba

NA DIRAMAKINI

MSANII maarufu wa muziki nchini Tanzania, Rajabu Abdulkahali Ibrahim maarufu Harmonize amethibitisha kudaiwa kodi ya nyumba kufuatia kusambaa kwa kipande cha video kinachomuonesha mwenye nyumba akilalamikia deni hilo.
Video hiyo iliyosambaa mitandaoni jana ilimnukuu mwenye nyumba akidai kuwa, msanii huyo bado hajalipa kodi yake. Tukio hilo limezua mjadala mpana miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Mapema leo, Harmonize ametumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha kuwepo kwa deni hilo, huku akieleza kuwa tayari amehamia katika makazi mapya yaliyopo eneo la Goba, jijini Dar es Salaam. Amesema,hatua hiyo imechukuliwa baada ya mwenye nyumba kumtaka kulipa deni hilo.

Katika maelezo yake, msanii huyo amesisitiza kuwa hajawahi kuwa na hofu ya madeni, akieleza kuwa ni sehemu ya maisha na mafanikio. Aidha, aliwahamasisha wafuasi wake kutokata tamaa wanapokabiliwa na changamoto za kifedha, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kupambana.

Harmonize alibainisha kuwa,katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita amewahi kukopa na kulipa madeni mbalimbali yenye thamani kubwa, ikiwemo mikopo ya kampuni ya muziki, taasisi za kifedha pamoja na watu binafsi.

Hata hivyo, alidai kuwa licha ya uwekezaji mkubwa alioufanya katika lebo yake ya muziki, hajapata faida yoyote hadi sasa.

Mbali na hilo, msanii huyo alieleza kuwa amefanikiwa kujenga msingi imara wa kifedha, akitaja uwekezaji wake katika mali mbalimbali ikiwemo nyumba na magari ya kifahari, pamoja na thamani ya kazi zake za muziki.

Katika ujumbe wake, Harmonize pia aligusia umuhimu wa kuthamini watu wanaosimama bega kwa bega katika nyakati ngumu na nzuri, akiwashukuru baadhi ya watu aliowataja kuwa wamekuwa msaada mkubwa katika maisha na safari yake ya muziki.

Tukio hilo linaendelea kuvuta hisia za wadau wa burudani, huku likifungua mjadala kuhusu changamoto za kifedha zinazoweza kuwakumba hata wasanii wenye mafanikio makubwa.

Ameandika Harmonize...

''yess wadau kama mlivyosikia kwamba nadaiwa kodi ya nyumba baba mwenye nyumba kanijia juu now imenibidi nifungashe uzuri nimepata nyumba kali tuu maeneo ya goba huku ..!!

"binafsi sijawahi kuwa muoga wa madeni wala maisha, kama kuna mtuu anakudai au hata mtandao wa simu unakudai na unasoma hii post ..!!

"usirudi nyuma usijali hata kondeboy anadaiwa na nikukumbushe baadhi ya madeni niliyo pata & kuyalipa kipindi hiki hiki nikiwa napambania imani mliyonipa kwenye muziki isipotee ..!!!!
1️⃣ . label 600.m ✅
2️⃣. bank crdd 200m.
✅ 3️⃣ . dr jembe 100.m ✅
4️⃣ . sarah mzungu 180.m ✅
5️⃣ . invested over 1.b on the label ✅

"in 3 years i have got nothing …!! yani zero 0️⃣ haya machache kwa kuyatazama lakini mazito sana kuyatekeleza sina jasho la mtuu na hii imenifunza hakuna kitu cha bure & kutofautisha kati ya makubaliano na maridhiano sijawahi kuleta janja janja wala kutafuta kisingizio cha kudhurumu haki ya mtuu hakuna laana inayonipata ..!!!

"upendo na huruma yenu imeniwezesha .!! ❤️ please keep going ⬆️ siovizuri sana kujisifu mafanikio machoni pa watu ndiomaana huwa nanyamazaga hata lisemwe nini ila wewe jua kwamba nimefanikiwa kimaisha mapema mno kuringanisha na mimi wa zamni parking yangu ina thamani ya 2.b yani v8 2 range rover sport 1 range rover defender 2024 1 bmw 4z 1 invested on mansion houses than 4.b my music catalogue ina thamani ya 5.m usds nikisema niiuze leo..!!!!

"sina mkopo wala marejesho yoyote ✋ anyways jana mvua ilichapa sana kipande cha goba, bubaaa…!! nikakutana na @_kusah_ mazungumzo yetu yalijikita zaidi katika kutambua mchango & thamani ya watu tulio nao wanao jitoa usiku na mchana kwaajili yetu …!!! nyakati hizi mambo ni mengi sana..!!!

"hata ufanye nini unahitaji mtuu sahihi pia ni rahisi sana hasa kwasisi vijana kujisahau na kumchukulia poa ulie nae for some time ..!! imagine mama mtu kakubali tuhamie zetu goba …!!

"hana noma share this to someone unaemuamini kwamba anaweza simama na wewe katika nyakati zotee 🙏 mwabie kama sio wewe !!!! nisingekuwa hapa..!!! kajalafrida & auntyezekiel nyinyi ni watu na nusu ..!!! mionekano yetu inajieleza zaidi ❤️❤️,''ameandika Harmonize leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here